Katika klipu ya video iliyosambazwa na televisheni ya Al Jazeera, Mufti Mkuu wa Libya Sheikh Sadiq al Ghariani, amesema vita baina ya Iran na utawala wa Kizayuni, kwa mtazamo wa Kisharia, ni mapambano baina ya Uislamu na ukafiri.
“Utawala wa Kizayuni wa Israel umevamia na kushambulia nchi ya Kiislamu ili kueneza dhulma na uhasama,” amesema Sheikh al Ghariani. Ameongeza kuwa, “Utawala wa Kizayuni, kwa uungaj mkono wa wazi wa madola ya Magharibi unatekeleza mauaji ya kigaidi, na kumtisha yeyote itakaye.”
Mwanazuoni huyo wa Kiislamu nchini Libya amesisitiza kuwa, nchi za Magharibi, pamoja na utawala wa Kizayuni, zinapanga njama dhidi ya Iran, ambayo ni nchi za Kiislamu na kwa msingi huyo hivi ni vita baina ya Uislamu na ukafiri. Amesema uvamizi huo ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya kujitawala na uhuru wan chi za Kiislamu.
Taarifa hiyo imekuja baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutekeleza hujuma ya kichokozi dhidi ya Iran Ijumaa iliyopita ambapo ulilenga maeneo ya kijeshi na kiraia ya Iran. Katika kujibu, Iran inaendelea kulipiza kisasi kwa kutekeleza Operesheni Ahadi ya Kweli III kwa kulenga ngome za kijesi na kijasusi za Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
342/
Your Comment